
Ni kweli kwamba, mapenzi yanatesa kuliko kitu chochote katika uso wa dunia hii. Ni mapenzi hayohayo ambayo yana nguvu na maumivu makali kuliko maumivu ya kitu chochote unachokijua chenye kusababisha maumivu.
Pia ni kweli wapo watu wengi wameumizwa na kuteswa na mapenzi. Wengine wanaendelea kuteseka na kuumia kila siku. Wengine wanatamani kuyaepuka ingawa hawawezi zaidi ya kupumzika kwa muda. Wapo wanaotamani kuyakimbia ila hayakimbiliki. Wengine wanatamani kujiua ila roho wa Mungu anawashindia.
Kisa cha msanii mrembo Zaidi aliyeamua kuanika siri ya mapenzi inayomtesa.
“Nilijitoa kiakili, Nikatoa mpaka mwili lakini bado” Zipporah akisimulia namna alivyojitoa juu ya mpenzi ambaye hakuona thamani ya penzi lake.
Usimchukie aliyekuumiza na kukutesa katika mapenzi, amini ni sehemu ya maisha yako, ulipaswa kuyapita.