155 views 43 secs 0 comments

Boti iliyozama ugiriki ilikuwa na watoto 100

In KIMATAIFA
June 15, 2023

Manusurika wa boti ya wavuvi iliyozama kusini mwa ugiriki katika mojawapo ya maafa mabaya zaidi ya wahamiaji barani ulaya wanasema karibu watoto 100 huenda walikuwa ndani ya boti hiyo

Takribani watu 78 tayari wamethibitishwa kufariki katika maafa hayo

Lakini wengine zaidi Bado wamepotelea baharini,huku ripoti zikisema kuwa Hadi watu 750 walikuwa ndani ya boti hiyo

Walinzi wa pwani wa nchi hiyo wamekosolewa Kwa kutoingilia kati mapema lakini mamlaka inasema maombi Yao ya misaada yalikataliwa

Waokoaji Bado wanatafuta manusura katika bahari ya ugiriki huku matumaini ya kumpata manusura Zaidi yakipungua

/ Published posts: 1215

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram