232 views 3 mins 0 comments

BANDARI KAVU KWALA KUONGEZA MAPATO

In KITAIFA
May 27, 2023

Meneja miliki wa Mamlaka ya Bandari, Alexander Ndibalema akizungumza na Waandishi wa Habari leo Mei 27, 2023

Serikali kupitia TPA imeamua kujenga Bandari Kavu eneo la Kwala “Quarantine” Ruvu. Katika awamu ya kwanza, Hekta 502 zimetwaliwa na TPA ikiwa ni sehemu ya Hekta 52,000 ya eneo linalomilikiwa na Serikali kupitia Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, ambapo kihistoria, eneo hili lilikuwa chini ya usimamizi wa “Tanzania Livestock, Marketing Company (TLMC) na baadaye kuwa chini ya Tanzania, Livestock Marketing Project (TLMP).

\"\"


Eneo la Bandari ya Kwala lilitolewa na Serikali kwa TPA ili kuendeleza miundombinu ya Bandari Kavu ikiwemo Yadi, Majengo, Barabara na Reli zinazounganisha Bandari hiyo na reli za TRC na barabara kuu ya Morogoro. Bandari ya Kwala ipo karibu na stesheni za Msuwa na Ruvu kwa reli (SGR na MGR) za TRC.
Ujenzi wa mradi wa Bandari Kavu ya Kwala umegawanyika katika Awamu mbili (2), zenye jumla ya gharama ya shilingi 83.246 Bilioni.

SHEHENA INAYOTARAJIWA KUHUDUMIWA KATIKA BANDARI KAVU YA KWALA
Bandari ya Kwala inayotarajiwa kuhudumia shehena ya makasha yanayokwenda nchi jirani, inakadiriwa kuwa na uwezo wa kuhudumia makasha 823 kwa siku, na hivyo kuifanya Bandari hiyo kuhudumia hadi makasha 300,395 kwa mwaka; sawa na asilimia 30 ya makasha yote yanayohudumiwa na Bandari ya DSM kwa sasa.

\"\"

FAIDA ZA BANDARI KAVU YA KWALA
Faida zitakazopatikana kutokana na ujenzi wa Bandari Kavu ya Kwala ni pamoja na zifuatazo;
(i)Kuongeza ufanisi na kiasi cha shehena inayohudumiwa katika Bandari ya DSM:-

(ii)Kuongezeka kwa mapato ya Serikali kupitia huduma zitolewazo katika Bandari za DSM na Kwala;

(iii)Itapunguza gharama za uendeshaji hivyo kuvutia wateja kutumia Bandari ya DSM;

(iv)Kuongeza ushindani wa Bandari ya DSM kikanda ukizingatia uwekezaji wa Bandari za nchi jirani katika Bandari Kavu;

(v)Kuimarika kwa shughuli za kiuchumi na biashara za mikoa ya DSM na Pwani kwa kupunguza msongamano wa magari uliopo sasa;

(vi)Kuimarishwa kwa usalama barabarani kwa kuwa idadi kubwa ya shehena ya Bandari ya DSM kutumia usafiri wa reli;

\"\"

(vii) Maisha marefu ya miundombinu ya barabara za mikoa ya DSM na Pwani;

(viii) Utaongeza ajira kwa wakazi wanaoizunguka Bandari Kavu ya Kwala na Taifa kwa ujumla; na
(ix) Ongezeko la viwanda katika eneo la Kwala vitakavyovutiwa na uwepo wa Bandari Kavu na usafiri wa uhakika kuelekea lango kuu la biashara nchini-Bandari ya DSM.

Ujenzi wa Bandari Kavu ya Kwala unatarajiwa kuongeza ufanisi wa Bandari ya DSM, ambayo ndio lango kuu la kibiashara nchini. Aidha, manufaa mtambuka ya Bandari ya Kwala yatapelekea Tanzania kufunguka kiuchumi hivyo, ushirikiano na wadau wote ikiwemo Kamati yako ni muhimu ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.