119 views 27 secs 0 comments

RAIS SAMIA AFANYA MABADILIKO YA UONGOZI, UHAMISHO NA UTEUZI

In KITAIFA
May 23, 2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya
mabadiliko madogo ya baadhi ya Wakuu wa Mikoa, uteuzi wa Mkuu wa Mkoa,
uhamisho wa Wakuu wa Mikoa na uteuzi wa Mkuu wa Wilaya kama ifuatavyo:

  1. Amemteua Mhe. Said Mohamed Mtanda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara. Mhe.
    Mtanda ni Mkuu wa Wilaya ya Urambo mkoani Tabora. Anachukua nafasi ya
    Meja Jenerali Suleiman Mungiya Mzee. Meja Jenerali Mzee atapangiwa
    majukumu mengine.
  2. Mhe. Queen Cuthbert Sendiga amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa
    Manyara. Mhe. Sendiga ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, anachukua nafasi ya
    Mhe. Nyerere ambaye amehamishiwa mkoa wa Rukwa.
  3. Mhe. Charles Makongoro Nyerere amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa
    Rukwa. Mhe. Nyerere ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, anachukua nafasi ya
    Mhe. Sendiga ambaye amehamishiwa mkoa wa Manyara.
  4. Amemteua Bw. Kenani Kihongosi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Urambo.
    Anachukua nafasi ya Mhe. Mtanda ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa
    wa Mara.
    Mabadiliko, uhamisho na uteuzi huu unaanza mara moja.
    Uapisho wa Mkuu wa Mkoa mpya utafanyika tarehe 24 Mei, 2023 saa 10:00 jioni,
    Ikulu Chamwino.

Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Iku
lu