VIPAUMBELE VYA MPANGO NA BAJETI YA SEKTA YA UJENZI NA
UCHUKUZI KWA MWAKA WA FEDHA 2023/24
Sekta ya Ujenzi
(i) Kuanza ujenzi wa miradi saba (7) ya barabara yenye jumla ya kilometa 2,035 kwa
kutumia utaratibu wa Engineeering Procurement Construction and Finance ( EPC+F).
(ii) Kuanza utekelezaji wa ujenzi wa barabara kutoka Kibaha – Chalinze – Morogoro
Expressway yenye urefu wa kilometa 205 kwa kutumia utaratibu wa kushirikisha
Sekta Binafsi (Public Private Partnership – PPP).
(iii) Kuendelea na ujenzi wa miradi mikubwa ya barabara katika maeneo mbalimbali
yenye jumla ya urefu wa kilometa 1,031.98.
(iv) Kuendelea na Miradi ya Ujenzi wa Barabara iliyosaniwa Katika Mwaka wa Fedha
2022/23 yenye jumla ya urefu wa kilometa 393.6
(v) Kuendelea na ujenzi wa madaraja makubwa mawili (2) ya JPM (Kigongo – Busisi,
Mwanza) na Pangani (Tanga) pamoja na kujenga madaraja mengine katika
maeneo mbalimbali nchini.
(vi)Kuanza utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa barabara zenye jumla ya urefu wa
kilometa 269.12 ambazo zinatarajiwa kusainiwa kabla ya mwisho wa mwaka wa
fedha 2022/23.
(vii) Kuendelea na utekelezaji wa mradi ujenzi wa uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa Msalato pamoja na Kuendelea na kazi za ukarabati na upanuzi wa
viwanja vingine vya ndege katika mikoa mbalimbali.
Mheshimiwa Spika, Miradi yote hiyo ya barabara na madaraja ikamilika itakuwa na
jumla ya kilometa 3,934.7 za barabara zilizojengwa kwa lami ambazo zitaongeza urefu
wa mtandao wa barabara za lami zilizopo sasa za kilometa 11,587.82 na kufikia
kilometa 15,522.52 ambalo ni sawa na ongezeko la asilimia 34.2
Sekta ya Uchukuzi
i. Mradi wa Uboreshaji wa Usalama wa Usafiri katika Ziwa Victoria – Shilingi
bilioni 1.73;
ii. Mradi wa Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam – Shilingi bilioni 93.80.
iii. Mradi wa Ukarabati wa Njia Kuu ya Reli Iliyopo (MGR) – Mradi wa Tanzania
Intermodal Railway II – Shilingi bilioni 11.72;
iv. Mradi wa Ujenzi wa Reli Mpya ya Standard Gauge – Shilingi trilioni 1.113;
v. Mradi wa Ununuzi wa Rada, Vifaa na Ujenzi wa Miundombinu ya Hali ya
Hewa – Shilingi bilioni 13.00;
vi. Mradi wa Uboreshaji wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) – Shilingi
bilioni 300.00;
vii. Mradi wa Ujenzi wa Meli Mpya na Ukarabati wa Meli – Shilingi bilioni
100.00;
viii. Mradi wa Kuboresha Miundombinu na Ununuzi wa Vifaa vya Kufundishia –
Shilingi bilioni 2.27;
ix. Mradi wa Uboreshaji wa Reli ya TAZARA- Shilingi bilioni 13.19; na
x. Mradi wa Ununuzi wa Mitambo ya Kuongozea Ndege na Uendelezaji wa
Chuo cha Mafunzo ya Usafiri wa Anga – Shilingi bilioni 6.5.
Katika mwaka wa fedha 2023/24, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi inaomba kuidhinishiwa
jumla ya Shilingi 3,554,783,957,000.00. Kati ya fedha hizo, Shilingi
1,468,238,449,000.00 ni kwa ajili ya Sekta ya Ujenzi na Shilingi 2,086,545,508,000.00
ni kwa ajili ya Sekta ya Uchukuzi.