134 views 5 mins 0 comments

420 WAPIMWA MOYO MANYARA

In KITAIFA
May 20, 2023

Baadhi wa wataalam wa afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Manyara (MRRH) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa kambi maalum ya siku tano ya matibabu ya moyo leo Mkoani Manyara. Jumla ya watu 420 wamefanyiwa uchunguzi na matibabu ya moyo katika kambi hiyo.

Jumla ya watu 420 wamefanyiwa uchunguzi na matibabu ya
magonjwa ya moyo katika kambi maalum ya siku tano iliyoanza tarehe 15 Mei
2023 na kumalizika leo katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Manyara (MRRH).
Kambi hiyo iliyofanywa na wataalam wa afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Manyara
(MRRH) imewahudumia watu wazima 390 na watoto 30.

\"\"

Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Mohamed Wamara akimpima kipimo cha kuangalia jinsi mfumo wa umeme wa moyo unavyofanya kazi (Electrocardiography – ECG) Glory Ifunya aliyefika katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Manyara (MRRH) kwa ajili ya kupima moyo wakati wa
kambi maalum ya siku tano ya matibabu ya moyo iliyokuwa ikifanywa na wataalam wa afya wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa MRRH na kumalizika leo Mkoani Manyara

Akizungumza wakati wa kufunga kambi hiyo Daktari bingwa wa magonjwa ya
moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Johnstone Kayandabila alisema
katika kambi hiyo wametoa rufaa kwa wagonjwa wa moyo 99 ambapo kati yao
wagonjwa 10 walikuwa watoto na wagonjwa 89 walikuwa watu wazima ili
waweze kufika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete kwa ajili ya matibabu zaidi.
“Sababu za kutoa rufaa kwa wagonjwa hao ilikuwa ni pamoja na matatizo
mbalimbali yanayotokana na athari za magonjwa ya shinikizo la juu la damu,
sukari kuwa juu, mishipa ya damu kuziba pamoja na valvu za moyo kutokufanya
kazi vizuri”.
“Magonjwa mengine tuliyokutana nayo wakati wa kambi hii ni matatizo ya mfumo
wa umeme wa moyo kutokufanya kazi vizuri na magonjwa ya moyo ya kuzaliwa
nayo kwa watoto yaani matundu kwenye moyo”, alisema Dkt. Johnstone
Aidha Dkt. Johnstone alitoa wito kwa wagonjwa waliopewa rufaa kufika JKCI ili
waweze kupatiwa matibabu kwa haraka kupunguza athari zitakazoweza
kujitokeza kama hawatapata matibabu kwa wakati.

\"\"

Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Johnstone Kayandabila akimpima kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanyakazi (Echocardiogram – ECHO) mwananchi wa Manyara aliyefika katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Manyara (MRRH) kwa ajili ya kupima moyo wakati wa kambi maalum ya siku tano ya matibabu ya moyo iliyokuwa ikifanywa na wataalam wa afya wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa MRRH na kumalizika leo Mkoani Manyara

Naye Mganga Mfadhiwi Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Manyara Dkt. Catherine
Magali amewapongeza madaktari bingwa wa moyo kutoka JKCI kwa kutoa
huduma kwa wananchi wa Manyara kwani huduma hizo ni muhimu kufanyika
mara kwa mara.

“Kuwapata watu 99 rufaa kwa wiki moja sio kazi ndogo, mmefanya kazi ya ziada
kwani watu hawa wangeendelea kuishi tu huku bila ya kujua yakuwa walihitaji
matibabu ya haraka kuokoa maisha yao”, alisema Dkt. Catherine
Dkt. Catherine ambaye pia ni bingwa wa magonjwa ya wanawake MRRH alisema
mwanzo wa ushirikiano uliojengwa katika kambi hiyo uendelee hata pale Hospitali
ya Rufaa Mkoa wa Manyara itakapowahitaji tena mabingwa hao kutoka JKCI
wasisite kushirikiana nao.

\"\"

Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Janeth Mmari akimfanyia uchunguzi mwananchi wa Manyara aliyefika katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Manyara (MRRH) kwa ajili ya kupima moyo wakati wa kambi maalum ya siku tano ya matibabu ya moyo iliyokuwa ikifanywa na wataalam wa afya wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa MRRH na kumalizika leo Mkoani Manyara

“Kuwapata watu 99 rufaa kwa wiki moja sio kazi ndogo, mmefanya kazi ya ziada
kwani watu hawa wangeendelea kuishi tu huku bila ya kujua yakuwa walihitaji
matibabu ya haraka kuokoa maisha yao”, alisema Dkt. Catherine
Dkt. Catherine ambaye pia ni bingwa wa magonjwa ya wanawake MRRH alisema
mwanzo wa ushirikiano uliojengwa katika kambi hiyo uendelee hata pale Hospitali
ya Rufaa Mkoa wa Manyara itakapowahitaji tena mabingwa hao kutoka JKCI
wasisite kushirikiana nao.