141 views 56 secs 0 comments

RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI

In KITAIFA
May 12, 2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amemteua Bw. Mussa Mohamed Makame, Mkurugenzi Mtendaji, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri na Uwekezaji wa Mfuko wa Mafuta na Gesi (Portfolio Investment Advisory
Board). Aidha, Mheshimiwa Rais amewateua Wajumbe wa Bodi hiyo kama
ituatavyo:-

  1. Dkt. Suleiman Magema Missango – Meneja Msaidizi Kurugenzi ya Utafiti na Sera, Benki Kuu ya Tanzania (BoT);
  2. Bw. Safiel Fahamuel Msovu – Afisa Fedha Mwandamizi, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC);
  3. Bw. Shogholo Charles Msangi – Mkurugenzi wa Kampuni ya Express Microfinance Company Ltd; na
  4. Bi. Mwanaidi Athuman Manda – alikuwa Mhasibu Mkuu wa Serikali.

Uteuzi huu umeanza tarehe 11 Mei, 2023.

\"\"