Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi, Sophia Edward Mjema akizungumza na Jukwaa la Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA) pamoja na vyombo vingine kama Magazeti, Televisheni na Redio ikiwa ni katika kuhakikisha mahusiano baina ya Chama Cha Mapinduzi na Wanahabari yanazidi kuwa bora. Mkutano huo ulifanyika Dar es Salaam Mei 11, 2023. |
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi, Sophia Edward Mjema leo amekutana na kuzungumza na Jukwaa la Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA) ikiwa ni katika kuhakikisha mahusiano baina ya CCM na Wanahabari yanazidi kuwa bora na kuendelea kuimarika, kulingana na mahitaji ya wakati.
“Ndugu zangu Wanahabari kwaza naomba niwapogeze kwa kazi nzuri ambayo mnafanya ya kuelimisha umma na kuedelea kutagaza mambo mengi ya Serikali inayoongozwa na Chama Cha Mapinduzi katika awamu hii ya sita ya Mhe. Rais wetu, Dkt. Samia Suluhu Hassan, niwapogeze na niendelee kushukuru kwa niaba ya chama kwa kazi ambazo mmekua mkizifanya,” alisema Mjema.
Aidha Mjema amesema tangu ashike wadhifa huo wa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi miezi minne na nusu sasa ameendelea kufaya kazi na Wanahabari kwa ukaribu japo siyo wote na kuahidi kendelea kufanya kazi pamoja na makundi mengi zaidi ya Waandishi wa Habari.
“Chama Cha Mpainduzi kitaendelea kutambua umuhimu na nafasi ya vyombo vya habari katika kueneza Sera na Itikadi ya Chama cha Mapinduzi na kuuhabarisha umma kuhusu utekelezaji wa Ilani ya CCM na utendaji kazi wa Serikali zake zote mbili, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar”, amesema.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa JUMIKITA, Shaban Matweve amemshukuru Mwenezi huyo wa Chama Cha Mpainduzi (CCM) kwa kukutana na Wana Habari wa Mitandao na kubadilishana mawazo, kitendo ambacho kimewapa faraja na kaihidi kuendelea kuzitangaza kazi nzuri zinazofanywa na Serikali ikiwemo miradi pamoja na chama kwa ujumla.
Mbali na JUMIKITA mkutano huo pia uliwakutanisha waandishi wa vyombo vingine vya Habari kama Magazeti, Televisheni na Redio nchini.